Psalms 78:54-68

54 aHivyo akawaleta hadi kwenye mpaka wa nchi yake takatifu,
hadi nchi ya vilima ambayo mkono wake wa kuume ulikuwa umeitwaa.
55 bAliyafukuza mataifa mbele yao,
na kuwagawia nchi zao kama urithi,
aliwakalisha makabila ya Israeli katika makao yao.

56Lakini wao walimjaribu Mungu,
na kuasi dhidi ya Yeye Aliye Juu Sana,
wala hawakuzishika sheria zake.
57 cKama baba zao, hawakuwa thabiti wala waaminifu,
wakawa wasioweza kutegemewa
kama upinde wenye kasoro.
58 dWakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia miungu,
wakachochea wivu wake kwa sanamu zao.
59 eWakati Mungu alipowasikia, alikasirika sana,
akamkataa Israeli kabisa.
60 fAkaiacha hema ya Shilo,
hema aliyokuwa ameiweka katikati ya wanadamu.
61 gAkalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani,
utukufu wake mikononi mwa adui.
62 hAliachia watu wake wauawe kwa upanga,
akaukasirikia sana urithi wake.
63 iMoto uliwaangamiza vijana wao,
na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi,
64 jmakuhani wao waliuawa kwa upanga,
wala wajane wao hawakuweza kulia.

65 kNdipo Bwana alipoamka kama vile kuamka usingizini,
kama vile mtu aamkavyo kutoka kwenye bumbuazi la mvinyo.
66 lAliwapiga na kuwashinda adui zake,
akawatia katika aibu ya milele.
67 mNdipo alipozikataa hema za Yosefu,
hakulichagua kabila la Efraimu,
68 nlakini alilichagua kabila la Yuda,
Mlima Sayuni, ambao aliupenda.
Copyright information for SwhNEN